Saturday, June 18, 2016

WAZIRI MKUU MH.KASSIM MAJALIWA AAGIZA MIKOA KUWA NA BENKI ZA WANANCHI

Waziri mkuu kassim majaliwa ameagiza kila mkoa kuweka mpango wa kuanziasha benki ya wananchi akitoa maagizo hayo jana akifungua mkutano wa wadau wa jumuiya za benki za wananchi unaofanyika jijini dar es salaam.

CHUCHU HANSY KUJA NA FILAMU MPYA IITWAYO USIKU WA DAKU

Msani filamu tanzania CHUCHU HANSY yupo mbioni kutoa filamu yake mpya iitwayo usiku wa daku akiongea na blog hii hapo jana chuchu alisema filamu hiyo imejikita sana kwemye maswala ya dini ya kiislamu hasa kwemye kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani pia amewaomba mashabiki wake wakae tayari kuipokea kazi yake hiyo mpya inayotarajia kutoka mwishoni wa mwezi huu .

Thursday, June 16, 2016

HAPPY BIRTHDAY MC VIOLETH KAPENJA.













MC VIOLETH KAPENJA akiwa na jopo la ma mc wenzake walipojumuika katika usiku wa birthday yake iliyofanyika katika hotel ya SELENA jijini dar es salaam tafrija hilo iliambatana na shoo kutoka kwa msanii wa bongo fleva linex sande mjeda na wasanii wengine kibao


FILAMU YA MSAMAHA INTERVIEW

Monday, June 13, 2016

WACHEZAJI WA YANGA WAKICHEZA WIMBO WA ALLI KIBA AJE

STEPS ENTERTAINMENT KUACHIA FILAMU YA MATALA TAREHE 20/06/2016


Kampuni ya steps entertainment inayijishughulisha na usambazaj wa filamu za kitanzania inatalajia kuzindua filamu ya MATALA sikuya jumatatu filamu hiyo iliyobeba mafundisho kibao na kuwataka watanzania wakae tayari kwa kuipokea filamu hiyo
MATALA ni sifa mwanau mwenye mke zaidi ya mmoja na si kwa mwanamke kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja . Na sifa mwanume kapewa na munguna pia matala huchangia kuvunjika kwa ndoa nyingi ,.Hii ni kwa mimi sijui kama na wewe hujuifuatilia kisa na mkasa utapata jibui.

NEEMA NDEPANYA ATOA MISAADA KWENYE KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA







RAMADHANI KAREEM.

TUNAPENDA KUWATAKIA WATANZAIA WOTE HASA NDUGU ZETU WAISLAMU MFUNGO MWEMA WA RAMADHANI.
RAMADHANI KAREEM.

Wednesday, June 8, 2016

KOCHA MKUU WA YANGA PLUIJIM AWACHIMBA MKWALA WACHEZAJI WAKE .




PLUIJIN alisema haoni kama kuna sababu yoyote ya chezaji kuchelewa kambini maana itakuwa ni utovu wa nidhamu maana hata yeye amaeamua kukatisha mapumziko yake na kurudi Tanzania kukiandaa kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika michuano hiyo.

HAPPY BIRTHDAY MR JOSEPH KUSAGA (CEO) CLOUDS MEDIA

Mwenyezi mungu akupe umri mrefu na moyo mkunjufu mnoonakutakia kheri ya siku yako ya kuzaliwa..happy birthday to you.
Like


MAMA AMTOBOA MACHO MTOTO WAKE WA KAMBO.

Mama wa kambo amtoboa macho mtoto wa kiume wa mume wake baada ya kuletewa amlee. Hii ni baada ya yeye kuzaa watoto wa kike hivyo kuona wivu na hasira kwa nini mume wake kamletea mtoto ambaye sio wakumzaa yeye ndipo alipo mtoboa macho mtoto huyo.

MTI WA MUEMBE WAZUA KIZAZAA HUKO TANGA.

Ni katika uwanja tangamano mkoni tanga imesemekana kuwa kuna mtu aina ya muembe kuonekana ni waajabu ambapo ifikapo majira ya jioni mwembe hubadilika taswira na kufanana na sura ya MWALIMU JULIAS NYERERE mti huo umekusanya watu kutoka katika maeneo tufauti ya mji wa tanga ili kuushuhudia .


Tuesday, June 7, 2016

KIKULACHO KIPO NGUONI MWAKO

​Ilikuwa kawaida yake kulala na nyoka wake, na haya ndiyo yaliyomkuta​

Hii ni hadithi ya kweli kuhusu mwanamke aliyekuwa na nyoka wake aina ya chatu aliyempenda
sana. nyoka alikuwa na urefu wa mita 4, aliishi naye kwa  muda mrefu na siku zote nyoka yule alionekana mwenye afya. Hata hivyo, nyoka alianza kukosa hamu ya kula kwa wiki kadhaa jambo lililomnyima raha mama yule kwani alihisi nyoka wake ni mgonjwa.  Mama alijaribu kumpa  kila kitu alichoweza ambacho nyoka wangependa kula lakini haikusaidia kitu, mama yule alikata tamaa na aliumia zaidi kwakuwa alimpenda sana nyoka wake.  Hatimaye mama yule aliamua kumpeleka nyoka wake kwa daktari wa mifugo. Daktari alimsikiliza yule mama kwa makini kisha akamuuliza , " Je, unalala na nyoka wako wakati wa usiku?  anapenda kulala karibu zaidi na wewe na kujipimisha urefu wake na wako? "
Mama kwa matumaini makubwa alisema, "Ndiyo! Ndiyo! anafanya hivyo kila siku na inanipa huzuni kwa sababu nahisi kuna kitu anatamani kuniambia lakini hawezi na Mimi pia nashindwa kumuelewa hivyo nakosa namna ya kumsaidia ili ajisikie vizuri kama siku zote "
Daktari akampa jibu la kushtusha moyo " Mama, chatu wako si mgonjwa ; ... "Ndiyo, chatu hakuwa mgonjwa, amekuwa katika maandalizi ya kumla mama yule. daktari akaendelea, "Kila wakati anataka kukaa karibu na wewe, kujikunjakunja mwilini mwako na kukutambaa kila muda, lengo lake ni kupima ukubwa wako na  kuangalia namna gani utakuwa mzuri mlo wake. anajilinganisha kujua jinsi gani utawa mlo mkubwa kwake hivyo anajipanga kwa mashambulizi. Na ndio maana hataki kula sasa ili kulipa tumbo lake nafasi ya kutosha kwaajili yako pindi atakapokugeuza kitoweo chake ".

​FUNDISHO​- Watu wako wa karibu zaidi unaowaamini, wapole na wanaoonyesha kukupenda wanaweza kuwa wabaya zaidi kwako. Upendo wa dhati na dhamira nzuri haitokani na namna watu wanavyo Kukumbatia na kukuchekea. Unafiki huambatana na Upendo wa kujilazimisha. Usiogope mashambulizi yanayopangwa na maadui zako juu yako Bali ogopa rafiki mnafiki anayekukumbatia na kukuchekea huku anakumwagia sumu kali. Adui wa MTU ni wa nyumbani mwake.

EDDY MASSE ENTERTAINMENT INAWATAKIA WAISLAMU WOTE MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KAREEM

Mwenyezi mungu awaongoze katika kipindi hiki na awafanyie wepesi.


ROSE NDAUKA KATIKA MAANDALIZI YA FILAMU YAKE MPYA YA ANGELA.

ROSE NDAUKA



Msanii wa filamu za kitanzania rose ndauka akiwa katika moja ya kipande katika filamu yake mpya iitwayo ANGELA .

HATIMAYE ABDALLAH KISANDA ALIYEKUWA MCHEZAJI WA JKT RUVU APATA JIKO..






Aliyekuwa mchezaji wa jkt ruvu abdallah kisanda fundi wa mpira mnamo siku ya jumamosi aliweka wazi na kumtambulisha mke wake ikiambata na harusi yao iliyofanyika maeneo ya mtoni kwa azizi ally harusi hiyo ilihudhuliwa na watu mbalimbali pamoja na wachezaji wenzake kumuunga mkono mwenzio walihudhulia katika sherehe hiyo ni alex joseph alimaluufu kama baba alice hamisi mpalu beki wa kulia wa yanga african U20 na wengine wengi pia kisanda amewashukuru sana wote waliohudhulia sherehe yake na kuahidi kurudi uwanja baada ya siku chache zijazo.

Monday, June 6, 2016

PACHA WA MSANII RIYAMA ALLY AITWAE MWANAHER KUACHIA FILAMU YAKE MPYA HIVI KARIBUNI.

MANAKHERI ndivyo wanavyo muita na wazazi wake msanii wa filamu hapa tanzania yupo mbioni kuanjia filamu yake mpya iitwayo MWANAHER filamu hiyo iliyobeaba manjonjo kibao na kuchezwa na mastaa kibao akiwemo pacha wake mkubwa riyama ally alisema mwanaher na kuwashukuru watanzania kwa kumpokea vizuri katika kazi zake zilizopita na kuwaahidi kusubili kazi yake mpya ianayokuja na kuwaahidi mashabiki wake kutowaangusha maana filamu ni nzuri na wataipenda.




MOJA YA VIPANDE KATIKA FILAMU YAKE MWANAHER








MSANII WA BONGO MOVIE RACHEL BITHULO AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO.

Msanii anayekuja juu katika tasnia ya bongo movie nchini jana akiongea na mwanablog alikanusha kuwa yeye hana mahusiano na maneno yanayo sikika ni uzushi yeye yupo makini kwa ajili ya kazi zake na si mambo mengine msanii huyo aliyecheza movie ya nimekosea wapi kama movie queen ambapo ameonyesha uwezo wa juu sana ambapo aliwatahadharisha walio juu kuwa wakae tayari kwani mambo ndo yameanza.







Friday, June 3, 2016

OMARY TEGO AWAZAWADIA MASHABIKI WAKE ZAWADI YA RAMADHANI KARIM.

Msanii wa miondoko ya taarabu omary tego yupo mbioni kuachia kibao chake kipya kinaenda kwa jina la RAMADHANI KARIM hii ni mahususi kwa mashabiki wake na mashabiki wa muziki tanzania kaa tayari kuipokea nyimbo hiyo na kuonyesha ushirikiano.


FILAMU YA MSAMAHA KUACHIWA RASMI NA STEPS SIKU YA JUMATATU.

Filamu mpya ya msamaha inatalajia kutoka siku ya jumatatu ya tarehe 06/06/2016 ambapo akieleza mtunzi wa filamu hiyo kuwa filamu imasheheni mastaa kibao wa bongo movie  hivyo watanzania wajiandae kuitafuta na aliongezea kuwa ndani ya filamu hiyo imebeba ujumbe mzima wa mwezi mtukufu wa ramadhani








RICH MAVOKO AULA MKATABA WASAFI CLASSIC.

 RICHARD MAVOKO AKIWA NA SIMBA DIAMOND PLUTNUM



HATIMAYE SNURA AJA NA MENDE BAADA YA CHURA KURUDISHWA MAJINI.

Msanii wa bongo fleva snura mushi yupo mbioni kuachia kitu chake kipya kiitwacho MENDE baada ya baraza la sanaa kuifungia kazi yake iitwayo chura .

 SNURA MUSHI


Wednesday, June 1, 2016

ROSE NDAUKA ATOA MACHOZI MISAADA KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA KILICHOPO KIGOGO.

Msanii wa filamu tanzania Rose ndauka siku ya jumamosi akiambatana na timu yake walitembelea kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo maeneo ya kigogo ambapo alijumuika na watoto hao katika chakula cha mchana na michezo mbalimbali ambapo ziara hiyo ya msanii huyo iliambatana na uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo ANGELA iliyotoka siku ya jumatatu inayosambazwa na steps entertainment.Msanii huyo aliwasihi watoto hao kuwa na nidhamu na kujituma katika masomo yao ili kuepukana na wimbo zima la umasikini linaloikabili nchi yetu


.